Hivi tunawezaje kuishi kwa matumizi yafuatayo kila mwezi? Fikiri;
1. Matumizi nyumbani; chakula, umeme, gesi, maji, soda/juisi za wageni.
2. Ada za watoto zinazolingana na za chuo kikuu
3. Matibabu hospitalini
4. Fungu la kumi na Zaka ya kanisani
... 5. Kupanda Mbegu/ Sadaka
6. Shukurani ya Neno
7. Tozo za Flying toilets (wazoa taka wa mikokoteni ambao huzitupa hapo hapo)
8. Madalali wa nyumba/viwanja
9. Pango la nyumba
10. Fremu ya biashara/ofisi
11. Mazakayo wa mitandao ya simu [airtime vouchers]
12. Mafuta ya gari/nauli za daladala
13. Walinda/waosha magari (oya sista/blaza, mdogo wako nipo apaaa)
14. Tozo za kuegesha magari
15. Makato ya Mikopo ya ofisi/benki na mikopo ya dukani na kulipia mkopo wa gari
16. Tozo za internet cafe ili uweze ku-surf
17. Rambirambi ya mfiwa mtaani kwetu
18. Harusi ya ndugu yako wa ukoo na zawadi
19. Sendoff ya mtoto ya mdogo wake rafiki yako na zawadi kitchen/bag party
20. Kumuaga mfanyakazi mwenzetu na zawadi
21. Michango ya komunio ya 1 & 2 na kipaimara
22. Michango ya besdei party/Kipaimara na zawadi
23. Ndugu wa kule kijijini
24. Mshahara wa Hausigeli na na hausiboi
25. Bodaboda, teksi na bajaj
26. Duka la dawa na madawa
27. Tuisheni ya mtoto na vitabu
28. Kuchangia wahanga wa mabomu na mafuriko.
29. Kwenda kumuona mtoto aliyezaliwa
30. Kununua CD/DVD ya Uzinduzi wa Kwaya yetu
31. Chakula cha mbwa/kuku/bata
32. Mchango wa Ujenzi wa Kujenga/Kupanua Kanisa
33. Kuchangia Uinjilisti misioni
34. Outing ya kitimoto na mitoko ya Mlimani City/Steers nk
35. Ujenzi wa Nyumba Mabwepande/Mbezi/kimara/Kibaha/Bagamoyo/moshono/kule ushagoo n.k
36. Kuendeleza shamba mkuranga/Bagamoyo/makete/misenyi/Marangu nk (linalotaka kutaifishwa kwa kutoendelezwa)
37. Viti Virefu/vifupi, soda/juicy moja moto moja baridi
38. Maji ya Traffik
39. Chai ya Nesi na Daktari
40. Kahawa ya Hakimu, Masijala, Traffic, Karani na PP
41. Vishoka waunganisha maji na umeme
42. Kidogodogo cha mjumbe na mtendaji wa mtaa
43. Posho ya wataalamu mbalimbali na huduma za ushauri
44. Michango ya maendeleo ya kata/vijiji/mitaa na michango ya vikundi vya kikabila/VICOBA/SACCOS
45. Mavazi je, saluni, mawigi, urembo,
Hivi hali inakuwaje? Tafakari....
....ndo maana Mungu anasisitiza tuutafute kwanza ufalme wake na mengine yote ni ziada kwani mbona ndege wa angani wanakula na kunywa bureeee sembuse sie tulio bora zaidi yao?!!!!
Posted in DJ Fetty