LAW OF QUEUE:
Ukibadilisha mstari unapopanga foleni ule uliouacha
unakwenda mbio zaidi.
------------------------------------------------------
LAW OF TELEPHONE:
Namba unayopiga kwa makosa daima haipo busy
-------------------------------------------------
LAW OF MECHANICAL REPAIR:
Mikono yako inapokuwa michafu pua inaanza
kuwasha ili uikune
------------------------------------------------
LAW OF THE ALIBI:
Ukimdanganya bosi kuwa umechelewa kwa sababu gari
lako limepata pancha kesho yake utapata pancha kweli
----------------------------------------------------
BATH THEOREM:
Ukishajitia maji tu simu itaanza kuita
-------------------------------------------------------
LAW OF ENCOUNTERS:
Uwezekano wa kuonekana na watu unaongezeka
unapokuwa
na mtu unayetaka usionekane ukiwa nae
----------------------------------------------------
LAW OF THE RESULT:
Unapojaribu kumueleza mtu kwamba mashine yako
imeharibika ukiwasha itafanya kazi
----------------------------------------------------
LAW OF BIOMECHANICS:
Sehemu inayowasha mwilini huwasha zaidi pale
ambapo huwezi kujikuna
--------------------------------------------------------------------
LAW OF COFFEE:
Ukikaa tu ofisini na kuanza kunywa kahawa yako bosi
atakuita na kukuchelewesha mpaka kahawa yako ipoe
No comments:
Post a Comment