KIJANA aliyewahi kupata umaarufu mkubwa nchini kwa jina la Rama ‘mla
watu’, Ramadhan Seleman anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji baada ya
kukutwa na kichwa cha mtoto, Salome Yohana (3) mwaka 2008, amepelekwa
Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma, kupimwa akili.
Habari kutoka Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam zinasema kuwa mtuhumiwa huyo amepelekwa Mirembe ili kufanyiwa uchunguzi wa akili yake.
Akizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, afisa mmoja wa Jeshi la Magereza Kanda ya Dar es Salaam amesema wamelazimika kumpeleka Rama katika hospitali hiyo ya akili kutokana na vituko vyake.

“Tumeona
ni heri tumfanyie uchunguzi wa akili kwa sababu ilikuwa ni vigumu
kuendelea na kesi mahakamani kutokana na vituko alivyokuwa akivifanya
tangu alipokamatwa.
“Miongoni mwa mambo yanayotatanisha ni pale alipokamatwa akiwa anakula kichwa cha mtu, hicho siyo kitu cha kawaida, hivyo ni muhimu kumchunguza akili yake kwanza.
“Tukishabaini tatizo ndipo tutajua jinsi ya kuiendesha kesi hiyo inayomkabili,” alisema afisa huyo.
Ramadhan na mama yake Khadija Ally wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya mtoto Salome yaliyotokea Aprili 26, mwaka 2008.
Mapema Oktoba 2011, Jaji wa Mahakamu Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Samuel Gibson Karua aliamuru mtuhumiwa huyo akapimwe akili katika hositali hiyo.

No comments:
Post a Comment