Friday, December 21, 2012

VIDEO INAYOONESHA SHAMSA AKIJIFUNGUA YAZUA KIZAAZAA






VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali.


Shamsa Ford.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo msanii huyo alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo.
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Shamsa ambaye alisema: “Kiukweli nimeumia sana, hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”

Monday, December 10, 2012

Jackline Wolper Amtambulisha Mchumba Wake Mpya Baada ya Kushindwana na Dallas




ALHAMISI iliyopita (Desemba 6, 2012), ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Jacqueline Wolper, jioni yake ndani ya Synergy Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam, alifanya bonge la pati, akiwaalika ndugu, jamaa, marafiki na majirani.

Mbele ya kila aliyehudhuria, Wolper alimtambulisha mchumba wake mpya ambaye amempiga bao, Abdallah  mtoro, ‘Dallas’ lakini akawaacha waalikwa na maswali lukuki pale alipogoma kumtaja jina.

Hakuishia hapo, akaomba mchumba wake huyo asipigwe picha hata ya kwenye simu, akisisitiza kuwa wana maana kubwa kuzuia hilo.


Mara nyingi mwenye fedha hata kama hasemi, vitendo vyake huongea, na kelele za jamaa huyo zilisomeka kwa herufi kubwa pale ulipowadia muda wa kumtuza ‘mtoto aliyezaliwa’ ambapo alimtuza cheni zenye thamani kubwa.

Wale waliomwakilisha jamaa huyo, hawakusema bei iliyonunuliwa, badala yake mmoja wao alitamka: “Cheni hizi zina thamani kubwa, kuliko zawadi yoyote ambayo inaweza kutolewa hapa.”

Cheni hizo ni mbili, moja ya shingoni na nyingine mkononi.


Mastaa kibao walihudhuria sherehe hiyo, kila mmoja alishangweka vya kutosha, huku misosi ikiwa siyo ya kuuliza, keki ilikatwa na kuliwa, shampeni zilifunguliwa na matukio mengine mengi ya kuvutia.

MC wa shughuli hiyo, Salum Mchoma ‘Chiki’, aliichangamsha sherehe na uwepo wa staa wa vichekesho, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, ulisababisha mbavu za waalikwa ziteseke.

Wolper, alipomtangaza mchumba wake huyo, alizungumza kwa kujiamini na madaha ndani yake na kusababisha wegeni wengi washangilie, huku wachache wakipigwa na butwaa.

Mmoja wa mastaa waliopigwa na butwaa, alihojiwa na ripota wetu na akajibu: “Kiukweli nilishangaa, unajua maneno yaliyokuwepo ni kwamba baada ya kuachana na Dallas angefulia lakini leo imekuwa tofauti ndiyo maana nimeshtuka kidogo.”

Staa huyo , alipoona atatafsiriwa vibaya, akaongeza kama aliyekumbuka kitu: “Lakini naomba ieleweke mshtuko wangu ni wa heri. Nampenda Wolper na namtakia maisha mema na huyo mchumba wake.”


Wapambe waliokuwa na mchumba huyo wa Wolper, walizungumza kwa kishindo ukumbini: “Kama kuna mtu alikuwa na mategemeo kwamba huyu mrembo atapata shida, hayo mawazo aondoe kabisa.

“Tunajua kila kitu kwamba Wolper alikuwa na mtu ambaye alishindwa kumgharamia, kwa hiyo hapa kafika. Tutamhudumia vizuri sana.”

 Kwa mjibu wa Wolper, sherehe hiyo imegharimu shilingi 19,600,000.

“Nawashukuru sana marafiki zangu waliokuja kunisapoti kwenye sherehe hii maana nimejisikia faraja ambayo sikutegemea kuipata kwa leo.

“Nimetumia milioni 19 na laki 6 kwa ajili ya kuandaa sherehe hii ili niwaburudishe marafiki  na ndugu zangu, ingawa kwa haraka haraka wengi ukiwatajia fedha hii wataona ni nyingi ila waliyokuwemo ukumbini wenyewe wataamini maana vinywaji na vyakula vyote vilikuwa vikitoka humo humo na hatukununua nje.”

CREDIT: GPL

Rihanna blasts Chris Brown as he parties with Karrueche in Paris



Rihanna was very angry after she found out Karrueche Tran joined Chris Brown in Paris and partied with him on Friday night after his concert.

She took to twitter and sent out a series of angry tweets that seemingly were aimed at Chris. She tweeted- Examine what you tolerate, Claps for the basic b**ches. See more below...

 
 
 

Chris Brown must have reached out to her to explain what Karrueche was doing with him in Paris because Yesterday night, Rihanna Tweeted a photo of herself lying in his arms with the caption,  
'Damn....... I miss my nigga #thuglife #BFFlif. See it after the cut...


RAY C AMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MSAADA WA MATIBABU ALIYOMPATIA...!!!




Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila 'RAY C' akimshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu aliompatia ikulu jijini Dar es Salaam leo. 

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
---
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

(Picha na Freddy Maro Ikulu)