Friday, November 16, 2012

MWIGIZAJI AUNTY EZEKIEL NA DEMONTE WAMEREMETA DUBAI...!!!

 
Mr & Mrs Demonte katika pose wakati wa reception yao
Mrs Rahma Demonte katika pose mara baada ya kufunga ndoa
Mrs Demonte akiwa katika pose na Milly Almasi
Sunday & Aunty wakilisakata rhumba

New couple in town
Aunty akiwa na mume wake na wapambe wao.
 
Source: jestinageorge blog

Wednesday, November 7, 2012

"MAMA USIJE KWANGU BILA TAARIFA.....VINGINEVYO WALINZI WATAKUTIMUA".......WEMA SEPETU


KITENDO cha staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu kuwaambia walinzi wake kuwa kama hajatoa maagizo yoyote kwamba mama yake, Mariam Sepetu anakuja, akifika mlangoni asifunguliwe kimewashangaza wengi.


Awali, Wema alieleza kuwa, ameweka utaratibu wa watu kuonana naye na kwamba wale watakaokwenda kwake bila taarifa watakuwa wanaishia getini.

Maelezo hayo yalimfanya mwandishi wetu amuulize kama hata mama yake akienda kwake bila ‘apointimenti’ hawezi kuingia ndani ambapo alisisitiza kwa kusema kuwa, utaratibu huo ni kwa watu wote akiwemo mzazi wake huyo.


“Akija bila taarifa hawezi kuingia ndani. Si yeye tu, hata dada yangu, rafiki yangu yoyote yule, meneja wangu hata wewe kama sijatoa maagizo kwa walinzi basi ujue utaishia nje na ukinipigia simu huwa sipokei,” alisema Wema.


Kauli hiyo iliwafanya baadhi ya watu kumshangaa kwa kusema kuwa, utaratibu huo si mzuri kwani kufikia hatua ya kumtaka hadi mama yake aweke apointimenti ndipo amtembelee ni kutafuta laana

Ndauka ajitetea kwa kirefu


MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Rose Ndauka amekanusha kuhusu madai kuwa amekuwa akiitisha usahili kwa wasanii Chipukizi na kuwachukulia fedha bila kuwashirikisha katika filamu zake.

Rose amekanusha shutuma hizo baada ya wasanii ambao waliwahi kufika katika ofisi za mwanadada huyo kushiriki katika usahili na kunyimwa nafasi.

�Jamani si rahisi kuchukua kila mtu anayeshiriki katika usahili inawezekana kweli akawa na sifa lakini wasanii wa aina hiyo wakawa wengi hapo linakuja suala la bahati ya mtu, hata wale wenye sifa majina yao yanahifadhiwa kampuni inapohitaji wasanii wengine wale ndio wanaopewa nafasi ya kwanza na si vinginevyo,� anasema Rose.

Siku za nyuma baadhi ya wasanii chipukizi walilalamika kuwa Rose amekuwa akifanya usahili kwa lengo la kujipatia fedha kwani mara nyingi baada ya usahili kufanyika wasanii ambao uwapanafasi ya kuigiza uwa ndugu zake na rafiki zake wa karibu na si walioshinda katika usaili, jambo lililomepingwa na Rose Ndauka