CHEGE APATA AJALI MBAYA YA GARI NA KUNUSURIKA...!!!
Hili ndio gari analolimiliki Chege mara baada ya ajali ambapo alikua na watu wengine ambao wote wamenusurika. Ajali
imetokea Temeke karibu na VETA Dar es salaam July 16 2012 usiku kati ya
saa nne na saa tano ambapo muendesha pikipiki aliingia ghafla
barabarani na ndio akawa chanzo, baada ya ajali yeye ndie alieumia
kuliko wenzake (mwendesha pikipiki). Chege kaumia mkono tu lakini mwenye pikipiki kalazwa Hospitali.
Msanii wa bongo flava Chege Chigunda usiku wa jana amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zimesema kuwa usiku huo Chege alikuwa ametokea jijini Nairobi.
Akiongea
na mtangazaji wa Clouds FM, Diva kwenye kipindi cha Ala za Roho, Chege
amesema usiku huo wa saa nne akiwa kwenye gari alikutana pikipiki katika
mtaa mmoja wa maeneo ya Temeke ambaye alimgonga na yeye kupata ajali
hiyo.
Chege amepata majeraha kadhaa lakini anaendelea vizuri licha ya gari lake kuharibika vibaya maeneo ya mbele. Haikuweza kufahamika mara moja hali ya mtu huyo aliyekuwa na pikipiki.
Kupitia mahojiano hayo mafupi Chege amewatoa hofu mashabiki wake kuwa hali yake ni nzuri na yupo salama.
No comments:
Post a Comment