Monday, December 31, 2012

WALIOTUSUA BONGO MOVIES 2012

 


WAKATI leo tukiufunga mwaka 2012, Ijumaa Wikienda linakudondoshea listi ya waigizaji wakali wa filamu za nyumbani waliofanya jitihada kwa kupiga mzigo hivyo kuibuka kidedea sokoni kwa muvi nyingi na kujiingizia mkwanja mrefu (kutusua).
 
Wema Sepetu.
Ifuatayo ni orodha ya mastaa 10 ambao wamefanya vizuri na kuuza filamu nyingi kuliko wengine ndani ya mwaka huu.
 
JACOB STEVEN ‘JB’Huyu ni mwigizaji mkongwe kunako gemu la filamu Bongo. Kupitia kampuni yake ya Jerusalem, JB anakiri kuwa ndani ya mwaka huu amefanya kazi nyingi. Amecheza filamu 23 na zote zipo sokoni na zinafanya vizuri katika mauzo tofauti na mwaka uliopita. Unaikumbuka DJ Ben?
 
STEVEN KANUMBA
Marehemu Steven Kanumba alitisha sana mwanzoni mwa mwaka 2012, kila mwezi alitupia kitu sokoni. Alipofariki dunia Aprili 7, filamu zake zote ziligombewa kama njugu sokoni. Filamu zaidi ya 10 ziliuzwa kwa kipindi hicho, mpaka sasa ile ya Ndoa Yangu ambayo ndiyo ya mwisho kuigiza, bado inatamba sokoni.
 
MZEE MAJUTOMwanzoni King Majuto alitisha kwenye filamu na maigizo ya kuchekesha. Ijumaa Wikienda linamzawadia nafasi kwa kuwa kila kona zilipouzwa filamu kulikuwa na muvi aliyocheza na biashara ilifanyika. Unakumbuka ripoti ya kutisha ya utajiri wake iliyotokana na kazi yake ya uigizaji? Mzee yupo vizuri.
 
VINCENT KIGOSI ‘RAY’
Nafasi hii tunaitoa zawadi kwa Ray kwani kupitia kampuni yake na mwigizaji Blandina Chagula ‘Johari’, RJ Production, aliweza kutengeneza filamu takribani 10 ambazo zipo sokoni na nyingine hazijatoka hadi sasa. Mzigo wa mwisho ni Waves of Sorrow, uliotanguliwa na Sister Mary.
 
DOKTA CHENI
Jamaa alifanya poa sana sokoni. Alikimbiza na anakimbiza na muvi kibao ambazo bado zinagombewa, mzigo wake wa mwisho ni Majanga.
 
WEMA SEPETUKwa upande wa wanawake, mwanadada Wema ameonekana kuuza katika filamu kibao ndani ya mwaka huu kwani wengi wanavutiwa na muonekano wake, hali iliyosababisha kufanya kazi zaidi. Ndani ya mwaka 2012 alicheza filamu zaidi ya 13 za watu. Mwisho akacheza moja ya kwake ya The Super Star aliyoizindua kwa kishindo kwa kumdondosha Bongo staa wa Nollywood, Omotola Jalade.
 
IRENE UWOYAHakuwa nyuma katika kufanya kazi japokuwa kuna kipindi alionekana kushuka kidogo. Baadaye filamu za watu alizocheza na za kwake zilikamata soko ghafla na kuwa gumzo kila sehemu zilipouzwa.
 
JACQUELINE WOLPERIjumaa Wikienda linamzawadia nafasi hii mwanadada huyu kwani kupitia kampuni yake alifanikiwa kutengeneza filamu saba ambazo zipo sokoni na nyingine kibao alizoshirikishwa na watu ambazo hakumbuki idadi yake.
 
MONALISA
Mwaka 2012 ulikuwa wa mafanikio kwa mwigizaji huyu kwani alipata tuzo ya msanii bora wa kike ambapo alicheza filamu kibao za kwake na nyingine zipatazo tano alishirikishwa na watu.
 
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’Kabla ya kukumbwa na mkasa wa kuhusishwa kwenye kifo cha Kanumba, Lulu alifanya poa sana mwanzoni mwa mwaka huu. Akiwa mahabusu, hivi karibuni ilitoka filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Dangerous Girl inayofanya vizuri sokoni.
CHANZO; GPL

No comments:

Post a Comment