Thursday, February 7, 2013

NDOA YA AUNT EZEKIEL "INAPUMULIA MASHINE"
KUMEKUWEPO na vijineno vya chinichini kuwa eti ndoa ya msanii maarufu wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel aliyofunga hivi karibuni na Sunday Demonte haipo na wabaya wake wamekuwa wakieneza taarifa hizo kwa kasi ya ajabu.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, watu waliodai ni mashosti wa karibu wa staa huyo walisema wamebaini dalili za wazi kuwa ndoa yake imeyeyuka.
“Mimi ndiyo nawaambia sasa, kama mlikuwa hamjui ndoa ya Aunt haipo. Fuatilieni mtabaini ukweli wa hiki ninachowaambia.

“Nyie si mjiulize mbona tangu amerudi kutoka Dubai hajaenda tena kumfuata huyo mumewe? Si alisema amekuja kuweka mambo yake sawa kisha anakwenda kuifurahia ndoa yake, kiko wapi sasa?” alihoji mmoja wa wanyetishaji hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.

Mwingine aliyekuwa mmoja wa waliofanikisha ndoa ya Aunt kwa kiasi kikubwa ambaye naye aliomba jina lake liwekwe kapuni alisema:
“Hata mimi nina mashaka na hii ndoa ya huyu mwenzetu, lakini iwe imevunjika, haijavunjika sisi haituhusu, kila mtu ana maisha yake bwana.”

Katika kujua ukweli wa madai haya, mwandishi wetu alimtafuta Aunt na alipotakiwa kulizungumzia hilo alisema:

“Tuna mipango yetu mimi na familia ndiyo maana Sunday yupo Dubai na mimi huku. Sipendi kuongelea mambo ya ndoa yangu magazetini lakini kwa kifupi ipo sawa.”

GLOBAL