Wednesday, November 28, 2012

WOLPER: NIKIACHIKA TENA, NATIMKA BONGO


PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa ughaibuni.

Wolper.
Akiteta na Tollywood Newz hivi karibuni jijini Dar, Wolper alisema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka tena kuwa na mpenzi wa Kibongo.
“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas’
.

Kim Kardashian topped the 2012 most-searched person on Bing

 
NEW YORK (Reuters) - Kim Kardashian topped the 2012 list of the most-searched person on Bing, the Web search engine said on Tuesday, with Canadian teen pop star Justin Bieber coming in second.
Kardashian, the reality television personality from "Keeping Up With The Kardashians," grabbed the No. 1 spot back from Bieber after she topped Bing's annual list in 2010 and Bieber came in first last year.
The 32-year-old first found fame in 2007 due to an Internet sex tape but it was her deft use of social networking and reality TV that propelled her into a global brand with various clothing lines, diet products and cosmetics.
Bieber, 18, came in second after a successful year capped off by sweeping the American Music Awards with his third studio album, "Believe," which was released in June.
Others who made it in top 10 for the first time included singers Rihanna, Selena Gomez, Nicki Minaj and Taylor Swift, while Jennifer Lopez, Britney Spears, Megan Fox and Lady Gaga dropped out of the top 10.
Pop culture figures easily trumped politics, even in an election year, with Republican presidential candidate Mitt Romney coming in 43rd and President Barack Obama landing at 46th on the list.
Among the most popular news stories, the release of Apple's iPhone 5 came in at No. 1, followed by the U.S. election, the Olympics and superstorm Sandy. The "Here Comes Honey Boo Boo" reality TV show landed at No. 5, followed by the "Gangnam Style Dance," popularized by South Korean rap star Psy's music video.
The birth of singer Beyonce and Jay Z's baby topped the most searched celebrity events, followed by Jessica Simpson's baby and then Whitney Houston's death.
 
Source:Reuters

Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA....!!!!! 

Habari zenye uhakika na zilizothibitishwa ni kwamba sharo milionea amefariki dunia leo hii usiku wa saa 2 kwa ajali ya gari huko MAGUZONI tanga na maiti iko katika hospital ya teule muheza, kwa habari za alieshuhudia ajali kulwa mbondei amesema marehemu alikuwa peke yake katika  ajali hiyo na alikuwa na gari aina ya HARRIER,Alisema gari iliacha njia na kuingia mapolini na kugonga mti baada ya hapo ilibingirika bingirika zaidi ya mara tatu na kupelekea kifo chake marahemu ameumia sana maeneo ya kichwani na jichoni .hapo ndipo wasamalia wema walipochukua simu yake nakuangalia majina ya watu kwenye simu nakumpigia simu TUNDA MAN kwamba sharo milionea amepata ajali na amefariki maiti ipo hospital ya teule muweza.hapo ndipo taaarifa za kifo cha sharo zilipoanza kusambaa. mungu mlaze mahala pema peponi SHARO MILIONEA


Monday, November 26, 2012

MSANII AFARIKI GHAFLA !!!!
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa akipanda juu kwa kasi, John Maganga (22) amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokimbizwa akiwa hoi, inasikitisha sana.

John Maganga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baba mdogo wa John, Deogratius Shija alisema Ijumaa iliyopita, marehemu alipatwa na maumivu ya ghafla ya tumbo, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu ya Mwananyamala, Dar ambako vipimo vilidai utumbo wa mgonjwa huyo ulitoboka.
Shija: “Daktari akatuambia kutokana na hali hiyo watamfanyia upasuaji ili kuuziba utumbo huo lakini mara baada ya zoezi hilo daktari akasema tatizo halikuwa kutoboka kwa utumbo bali kuna kitu kingine. 
“Ikabidi tumkimbize Muhimbili ambako madaktari wa pale walituambia wenzao wa Mwananyamala walikosea kumfanyia upasuaji John kwani tatizo halikuwa la kufanyiwa upasuaji bali alitakiwa apatiwe dawa.
“Madaktari wakatuambia tumwache pale ili waokoe maisha yake sisi ndugu turudi asubuhi. Tulipokwenda asubuhi tukaambiwa mgonjwa wetu alifariki dunia usiku uleule. Imetuuma sana.”      


Hivi karibuni, John aliandaa filamu yake ambayo aliipa jina la Beautfools ambayo yeye alicheza kama mume wa ndoa wa Aunt Ezekiel ambaye alimtenda John wakati anasoma chuo.
Marehemu alikuwa akienda vizuri katika tasnia ya filamu na ilisadikiwa angeweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. Kifo cha John kimeacha pigo kubwa Bongo Movies ambayo mpaka leo vilio vimetawala.
Mpaka jana Jumamosi, mazishi ya msanii huyo yalikuwa yakimsubiri mama yake mzazi aishie London Uingereza.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina

Monday, November 19, 2012

WAREMBO KUTOKA ULAYA KUSHIRIKI MISS EAST AFRICA 2012MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24).
MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24).
MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21).
Warembo mbalimbali wanaoishi Ulaya na walioshinda katika mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya pia watashiriki katika mashindano ya Miss East Africa 2012 yatakayofanyika tarehe 07 Desemba katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam warembo hao ni:
1. MISS EAST AFRICA BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
2.MISS EAST AFRICA NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
3.MISS EAST AFRICA FRANCE- Fiona Ruboneka (24)
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.

Embarrassment – Kate Middleton Returns Kim Kardashian’s Free Clothes!!Kate Middleton Returns Kim Clothes
Kate Middleton has returned clothes sent to her by Kim Kardashian. The British royal is known for championing high street as well as designer fashion, but didn’t accept a package sent by the reality TV star and her sisters Khloe and Kourtney from their new Dorothy Perkins range.
A source told The Examiner magazine: “Kate is hardly going to turn up for an event with the queen in a cheap leopard-print miniskirt or gold sequined jacket.”
Kim was also said to be keen to meet with Kate while she was recently in London, inviting her for tea.
A source said: “The Kardashians want to be as big in the UK as they are in America, and think associating themselves with the Royals, especially Kate, will help them achieve that. She hoped Kate might be seen wearing one of the designs out in public, which would give their fashion credentials a huge boost.”
Kim, 32, has been vocal about how much she loves Kate’s fashion choices in the past.
She said: “Kate seems like a really sweet person and she’s a princess. We love her sense of fashion. She could wear our looks and team it with one of her hats.”A representative for the Duchess made clear most gifts she is sent are returned.
By AHLAN! REPORTER

DAVINA AFUNGA NDOA .... !!!!
STAA wa filamu aliyewahi kutamba na Kundi la Sanaa la Kaole la jijini Dar, Halima Yahaya ‘Davina’ Alhamisi iliyopita alifunga ndoa kimyakimya na mwanaume ambaye mpaka sasa hajaamua  kumuweka hadharani, Ijumaa Wikienda linakujuza.
Halima Yahaya ‘Davina’ akiwa kwenye pozi siku ya ndoa yake.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Davina alifunga ndoa hiyo bila ya wasanii wengi kujua na walipopata taarifa walipigwa na mshangao mkubwa.
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Davina na kumuuliza kama ni kweli amefunga ndoa ambapo staa huyo alikiri na kusema kuwa wahudhuriaji walikuwa wachache kwa kuwa ndivyo walivyopanga.
“Walikuwepo ndugu na marafiki wa karibu, hata hivyo, maandalizi makubwa ya sherehe yanakuja, hivyo nadhani wengi nitawaambia,” alisema Davina.
...akiwa katika picha na mawifi zake.
Pia, Davina alifunguka kuhusiana na bifu lake na staa mwenzake Salama Salmin ‘Sandra’ na kusema msanii huyo anamchukia kwa kuwa alimkataza kuongea pembeni na mwanaume aliyefunga naye ndoa kipindi walipokuwa wachumba.
“Siku moja tulitoka na mchumba wangu (sasa mumewe) pamoja na Sandra ili kupata chakula cha jioni, Sandra akawa anataka kuongea pembeni na mchumba wangu jambo ambalo sikulipenda hata chembe, nikamkataza ndiyo akakasirika,” alisema Davina.
...mrembo Davina alivyokuwa ameng'ara siku hiyo.
Staa huyo alisema kuwa siyo kweli kwamba Sandra ndiye alimuunganishia mwanaume huyo aliyefunga naye ndoa, bali alijuana naye tangu alipokuwa Kaole na mwanaume huyo akiwa nje ya nchi.
“Sandra alifanya jitihada nyingi kuweza kuharibu uhusiano wetu lakini imeshindikana, hicho ndicho chanzo cha ugomvi wetu,”alidai Davina.
Staa huyo alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpata mwanaume wa maisha yake.
..pozi la bibi harusi hilo.

Chanzo: globalpublishers