KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Patrick
Mutesa Mafisango wa Simba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa
ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar es Salaam. Mafisango
amefariki kwa ajali ya gari akiwa anarejea nyumbani kwake, kutoka disko
na kwa sasa mwili wke upo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es
Salaam.
Meneja wa Simba SC, Nico Njohole
amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na amesema hilo ni pigo kubwa kwa
klabu hiyo. Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam
kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 Rwanda
na kabla ya Tanzania alichezea APR ya Rwanda.
Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea SImba
ilikuwsa dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya
Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia
sare ya jumla ya 3-3. Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo
na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange Kaburu alisema
kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao.
Poleni wana Simba wote, pole kwa ndugu,
jamaa na familia ya Mafisango. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake
lihimidiwe milele. Amin. Mungu iweke pema peponi Roho ya Marehemu.
Hivi ndivyo gari ya Marehemu Patrick Mafisango ilivyokuwa mara baada ya kupatwa na ajali na hatimae kupelekea kifo chake,Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Tutazidi kufahamishana kadiri ya habari zitakavyokuwa zikiingia.
chanzo:kajunason blog
No comments:
Post a Comment