LINGINE limeibuka! Kuna madai kwamba chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu kilipenyezwa kwenye Gereza la Segerea, Dar es Salaam, mlengwa wa kukila alikuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’,Kwa mujibu wa chanzo chetu, kijana kutoka Mwanza anayekadiriwa kuwa na miaka 18-20 anatajwa kuhusika na ubebaji wa chakula hicho ambacho hadi sasa haijajulikana nani amesimama nyuma ya zoezi hilo.
HABARI KAMILI
Habari zinasema kuwa siku chache zilizopita kijana huyo akiwa na mfuko wa rambo wenye chakula hicho alifika gerezani hapo na kufanya ujanja wa kuingia ili kumpa chakula Lulu.“Huyu kijana alipofika hapa alitumia ujanja wake akaingia ndani kwa lengo la kumpa chakula Lulu akijifanya ametumwa na familia,” kilisema chanzo cha ndani.Inadaiwa kabla hajafika kwenye eneo la kukutana na Lulu, maafande walio macho muda wote huku wakizingatia maadili ya kazi, walimnasa kijana na kumbana kwa maswali ambapo alishindwa kujibu na kuingia mitini.“Kabla hajamfikia Lulu yule kijana alidakwa na maafande wa pale Segerea, akapigwa maswali, lakini baadaye akaingia mitini. Nadhani alijua kiwewaka. Hapo ndipo alipotiliwa shaka kuwa huenda chakula chake hakikuwa na usalama ndani yake na huenda kilikuwa na sumu,” kilisema chanzo hicho.
KINGEANGAMIZA WENGI
Kwa mujibu wa habari za ndani kutoka jeshi la magareza, raia anapotumikia kifungo kuna watu wake watatu tu, wenye picha za vipande (passport size) ndiyo wanaoruhusiwa kumpelekea chakula.Sheria ya magereza inafafanua kwamba kabla mfungwa hajakula chakula alichopelekewa, mpelekaji anatakiwa kuwa mtu wa kwanza kukionja ili kuondoa shaka kama kitakuwa na kitu kibaya kwa hiyo kijana huyo angetakuwa kula kabla ya Lulu.“Unajua yule kijana kama kweli alitumwa kumwingizia Lulu chakula chenye sumu, basi aliingizwa mkenge, maana kabla ya kumpa Lulu ale, angetakiwa kula yeye kwanza, sasa si angekufa!“Mbaya zaidi, chakula hicho kingeendelea kutoa madhara kwa wengine maana kuna wafungwa huwa wanasaidiana chakula. Kwa hiyo unaweza kuona ni jinsi gani chakula kile kama kilikuwa na sumu kingeleta madhara makubwa,” kiliongeza chanzo.
NDUGU WAPONGEZA
Jumamosi (juzi) gazeti hili lilimsaka mama Lulu (Lucresia Karugila) kwa kupitia simu yake ya mkononi, hakupatikana lakini ndugu mmoja wa Lulu ambaye aliomba hifadhi ya jina alisema ndugu wamewapongeza maafande wa magereza ya Segerea kwa sababu walimudu vyema kumdhibiti kijana huyo.Hata hivyo, ndugu huyo alisema hakuna ushahidi wa moja kwa moja kama kweli chakula hicho kilikuwa na sumu kwani wapo wanaoamini kuwa, kijana huyo ni shabiki mkubwa wa Lulu kwa hiyo aliamini kumpelekea chakula ni sehemu ya kutoa hisia za mapenzi yake.
KWA NINI KIWE NA SUMU?
Ndugu huyo aliendelea kudai kuwa sumu ilidhaniwa kuwepo kwa sababu toka Lulu ashikiliwe na vyombo vya sheria kwa madai ya kujua chochote kuhusu kifo cha Steven Kanumba, amekuwa akipewa ulinzi mkali kwa sababu ya mitazamo ya baadhi ya watu kwamba staa huyo ndiye aliyemuua Kanumba.
JESHI LA MAGEREZA LINASEMAJE?
Baada ya kupata taarifa hizo, Julai 24, mwaka huu waandishi wetu walifika Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania, jijini Dar na kuzungumza na msemaji wa jeshi hilo, Omary Mtinga kwa lengo la kutaka kujua anasemaje kuhusu madai hayo.Hata hivyo, msemaji huyo alisema jeshi lake halina taarifa hizo lakini akaomba apewe muda ili aweze kuzifuatilia.Julai 28, mwaka huu, paparazi wetu alimpigia simu msemaji huyo na kumkumbushia kuhusu ahadi yake, lakini akasema yuko safarini nje ya jiji la Dar na alitarajia kurudi wiki inayoanzia leo.Lakini kwa msisitizo mkubwa Afande mtinga alisema aliwatuma vijana wake wa makao makuu kufanya upelelezi mkali gerezani Segerea, kwa hiyo akirudi atapata jibu na kuyaweka wazi.Akaongeza: “Lakini kama ni kweli ni kosa kubwa, mtu hawezi kupita bila utaratibu. Kila mfungwa ana utaratibu wa watu watatu kumpelekea chakula gerezani. Hata huyo (Lulu) ana watu maalum watatu wakiongozwa na mama yake mzazi ndiyo wanaoruhiswa kumpelekea chakula.”
No comments:
Post a Comment