Tuesday, August 7, 2012

MASANJA MKANDAMIZAJI ADAIWA KUTANDIKWA MAKOFI


MCHEKESHAJI wa Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’, mwishoni mwa wiki iliyopita anadaiwa kutandikwa makofi hadharani na polisi baada ya kuingilia msafara wa gari lililokuwa limebeba fedha.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea kwenye njiapanda ya Chalinze mkoani Pwani ambapo msanii huyo alikuwa akitokea Dar kuelekea Tanga huku akiendesha gari kwa kasi ya ajabu.


Chanzo hicho  kilieleza kuwa jamaa huyo alikutwa na kasheshe hilo baada ya ‘kuliovateki’ gari hilo lililokuwa likisindikizwa na polisi ambapo pamoja na kuzuiwa na wajeda hao, Masanja alijitoa fahamu na kujifanya kichwa ngumu.


Kilisema: “Baada ya ‘kuwaovateki’ wale polisi, ndipo nao (askari) wakamkimbiza hadi wakamkamata na ndipo akala mbata zake na soo likahamia kwenye Kituo cha Polisi cha Chalinze Njiapanda na kumshikilia kwa muda kisha kumuachia baada ya mahojiano.”


Ili kupata mzani wa habari hiyo, mwandishi wetu  alimtafuta Masanja ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kukamatwa na askari kutokana na makosa ya barabarani kwake ni suala la kawaida huku akikanusha kupewa kibano.

No comments:

Post a Comment