Sunday, April 15, 2012

HUDUMA YA KUTOA FEDHA M-PESA YAPUNGUA HADI ASILIMIA ISHIRINI

HUDUMA YA KUTOA FEDHA M-PESA YAPUNGUA HADI ASILIMIA ISHIRINI


Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20 ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala yeyote wa m-pesa.
Gharama hizi zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya Vodacom M-PESA .
“Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ”, alisema Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za kutoa fedha. ‘Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi” alisisitiza Bw. Meza.
Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya Kampuni kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo ‘tuma na ushinde’ ambapo shilingi milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni.
Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.
Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya bili kama vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA. Vilevile inaweza kutumika kulipia tiketi, safari za ndani za ndege za Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za shule, kuweka na kutoa fedha kupitia Benki ya CRDB, Western Union na huduma zingine nyingi.
Vodacom m-pesa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka kwambaVodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na matumizi ya kuongezekasiku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa masuala ya fedha hapa nchini.

Imetolewa kwa niaba ya:
Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Mahusiano na Mauzo kwa wateja wakubwa
Vodacom Tanzania Limited
Tel: Tel: +255754704265
Maulizo kwa ajili ya vyombo vya habari:
Matina Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited
+255755484800

No comments:

Post a Comment