Sunday, April 22, 2012

JACQUELINE WOLPER ABADILI DINI SASA ANAITWA ILHAMMsanii wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amebadili dini na kuwa Muislam baada ya kuchumbiwa na kununuliwa gari la kifahari na mwanaume anayeitwa Dulla au Dallas, Ijumaa linakupa habari hii kwa undani zaidi.
Kwa mujibu wa habari zilizotua katika meza yetu na kuthibitishwa na msanii huyo, Wolper amebadili dini katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na sasa atakuwa akitambulika kwa majina ya Ilham Wolper Dallas.
“Ni kweli nimebadili dini wiki mbili zilizopita baada kumpata mchumba ambaye tunatarajia kufunga ndoa hivi karibuni,” alisema Wolper.
Aidha, msanii huyo amesema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kumchunguza kwa muda mrefu mchumba wake huyo na kugundua kuwa ana nia nzuri kwa upande wake hivyo kukubali kumfuata katika dini yake.
Pia, Wolper amesema kuwa yeye na mchumba wake huyo wameshaanza kufanya taratibu za kupata baraka za wazazi wa pande zote mbili ili kuweza kufanikisha azma yao ya kufunga ndoa.
“Dallas ameshafika kwa wazazi wangu na hata mimi nimeshaenda kutambulishwa kwao, kilichobaki ni kufunga ndoa tu,” alisema

Wolper kwa kujiamini.
Baada ya Wolper kubadili dini na kukubaliana na mchumba wake kufunga ndoa, mwanaume huyo alijikunja na kumnunulia msanii huyo gari la kifahari aina ya BMW X6 ambalo anatanua nalo mitaani hivi sasa.

No comments:

Post a Comment