Monday, April 30, 2012

VIJANA VYUO VYA ELIMU YA JUU WATINGA CCM KUFIKISHA UJUMBE WAO KUHUSU MAFISADI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwapokea Vijana wa Shirikisho la Vijana wa CCM walioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika kwenye ofisi za Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo kuonana naye ili kufikisha msimamo wao kuhusu Mawaziri na Maofisa wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa fedha za umma. Vijana hao walookuwa na mabango yenye ujumbe mbali mbali pamoja na mambo mengine wamemuomba Rais Kikwete awachukulie hatua wahusika wote kwa kuwaondoa kabisa kwenye nafasi zao na si kuwahamishia kwingineko na kisha wachukuliwe hatua za kisheria, Kauli ambayo Nape aliwaunga mkono akiahidi kufikisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete.
Nape akizungumza na Vijana hao
Nape akisoma ujumbe kwenue moja ya mabango waliyofika nayo vijana hao
Kisha akasoma na mango hili
Vijana wakionyesha moja ya mabango waliyofika nayo
Na hili likieleza maana ya Mapinduzi
Hili likawataka ‘magamba’ wanaoondoka CCM wazidi kutimka.
Chanzo:http://bashir-nkoromo.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment