Thursday, August 16, 2012

" KAMA BUSHOKE ATANIZINGUA, BASI NITAITOA HII MIMBA"....JINI KABULA


SIKU chache baada ya kuripotiwa kuwa amenasa mimba, mwigizaji anayewakilisha Kundi la Scorpion Girls, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amemtaja mwanaume anayeitwa Bushoke kwamba ndiye baba wa mtoto wake.


Jini Kabula aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam baada ya kubanwa na waandishi wetu kufuatia madai kwamba, mwanaume aliyempachika mimba ni mfanyabiashara wa madini.


Hata hivyo, staa huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema ‘anampeleleza’ Bushoke kama kweli ana nia na mtoto atakayezaliwa au maneno maneno tu.

Alipobanwa kuhusiana na taarifa zilizowafikia wandishi wetu kuwa ana mpango wa kuitoa mimba hiyo, Jini Kabula alifunguka:


“Hii mimba ni ya miezi minne sasa, kama Bushoke hatakuwa na usumbufu wowote basi nitamzalia mtoto mzuri ambaye naye atatamba naye mitaani, lakini akinizingua wakati wowote, sikawii kubadili mawazo na kuichoropoa.”


Jini Kabula alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na bosi wa Kampuni ya Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ na kuzaa naye mtoto mmoja.


Aidha, ameshawahi kuwa na uhusiano kama huo na staa wa Bongo Fleva, Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’ lakini hawakubahatika kupata mtoto hadi walipomwagana
.

No comments:

Post a Comment