Raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki Emrah Erdogan (24) (Pichani) amekamatiwa nchini Tanzania kwa tuhuma za kufanya shambulizi la kigaidi mwezi ulopita mjini Nairobi, Kenya.
Inasemekana Erdogan aliingia Kenya mwezi mei 2012 akitokea nchini Somalia ambako amekuwa akifanya mashambulizi mbalimbali na kikundi cha kigaidi cha Al-shabab.
Kamishna msaidizi wa Polisi Tanzania amewambia waandishi kuwa Erdogan alikamatwa jijini Dar-es-salaam siku ya jumatatu tarehe 11 Juni.
Emrah Erdogan ambaye pia anatumia jina la Salahuddin al-Kurdi, tayari amefanyiwa mahojiano na taasisi za usalama kutoka Tanzania, Germany, Kenya naUganda.