Thursday, June 14, 2012

MASHUJAA YAMKANA KALALA JUNIOR

Mkurugenzi wa bendi Mashujaa inayofanya vizuri kwenye anga ya muziki wa dansi bongo Maxmilian Luhanga amesema uongozi wa bandi hiyo hauhusiki kwa namna yoyote na kujiweka kando kwa nyota wa muziki huo Kalala Junior wa Mapacha Watatu,
kuwa hakuna uhusiano wowote baina ya kuondoka kwa mwanamuziki huyo kwenye hiyo na kuwa taarifa zinazozagaa mjini kuwa Kalala Junior yuko kwenye mpango wa kujunga na Mashujaa bendi hazina ukweli wowote.
“Hakuna ukweli wowote kwenye taarifa hizo, kama Mashujaa, hatuhusiki kwa lolote na kuondoka kwake na hatujawahi kufikiria kumjumuisha kwenye kikosi chetu kwa sababu tunaamini bado hana nafasi hiyo kwa sasa kwa kuwa tuna waimbaji wanaojiweza na wakali zaidi” alisema Max.
Katika hatua nyingine Max aliongeza kuwa endapo mwanamuziki huyo ataomba kujiunga na bendi yao basi uongozi wa bendi utakaa kikao kuona kama ana nafasi na pengine anaweza kuruhusiwa kujiunga. alimaliza Max.
 Chanzo:teentz.com

No comments:

Post a Comment