Mmoja
wa waratibu na jaji, Isakwisa Thomson akikabidhi kitita cha shilingi
milioni moja kwa kundi kinara la Questions Crew kati ya saba
yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta
2012,lililofanyika jioni ya leo ndani ya kiota cha mangoma cha
Lakasachika mkoani Tanga.
Mmoja wa waratibu na jaji,Isakwisa Thomson akiwa na kitita cha fedha taslim sh milioni moja,kwa ajili ya kukabidhi kwa kundi la Questions Crew lililoibuka
mshindi wa kwanza kati ya makundi saba yaliyojitokeza kushiriki
shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,lililofanyika jioni ya leo
kwenye ukumbi wa Lakasachika mkoani Tanga.
Baadhi ya wacheza shoo wa kundi la Questions Crew wakizungumza machache mara baada ya kukabidhiwa kitita chao cha shilingi milioni moja
Baadhi
ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti-Tanga wakikabidhi Kreti
moja ya bia ya Serengeti ikiwa ni sehemu ya zawadi kwa kundi la Questions Crew mara baada ya kuibuka washindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012 mkoani Tanga.
Watu mbalimbali wakifuatilia shindano hilo.
Kundi
la Sweet Girls likionesha umahiri wake kucheza kwenye shindano la
kulisaka kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta 2012
Kundi
la la Street Colour likionesha umahiri wa kucheza mbele ya sehemu ya
wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza jioni ya leo kushuhudia shindano
la Serengeti dance la Fiesta lililofanyika ndani ya ukumbi wa
Lakasachika
Kundi la Questions
Crew likicheza kouwania kitita cha milioni moja kilichotolewa na
kampuni ya bia ya Serengeti sambamba na kreti moja ya bia.
Mdau Thomson akikata kiu yake safi kabisaa.
Palikuwa hapatoshi leo ndani ya ukumbi wa Lakasachika.
Pichani
juu na chini Sehemu ya wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga waliojitokeza
kushuhudia shindano hilo lilovuta hisia za vijana wengi
Mmoja wa majaji wa shindano hilo B Dozen akifafanua jambo wakati wa kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.
Mmoja
wa majaji wa shindano hilo Isakwisa Thomson akifafanua jambo wakati wa
kumsaka kinara wa mashindano hayo kwa mkoa wa Tanga.
Majaji
wa shindano la Serengeti dance la fiesta 2012 wakijadiliana jambo
wakati shindano likiendelea ndani ya ukumbi wa Lakasachika jioni ya
leo,ambapo wakazi mbalimbali wa jiji la Tanga walijitokeza kwa wingi na
kujionea vipaji.
No comments:
Post a Comment