Monday, August 13, 2012

NAOMI CAMPBELL KANYONYOKAJE NYWELE... !!!


 
 BAADA ya kuonekana mrembo kwa miaka mingi, mwanamitindo mkongwe Naomi Campbell, wiki iliyopita aliwashangaza wengi baada ya kubainika kuwa sehemu kubwa ya nywele zake kichwani hasa sehemu ya mbele zimenyonyoka na anastiliwa zaidi na nywele za bandia.
Picha za muonekano wa modo huyo mwenye umri wa miaka 42 zilinaswa wiki iliyopita alipokuwa amemaliza kuogelea katika pwani ya Ibiza.
Mara baada ya kutoka kwenye maji, muonekano wa kichwa chake kilicho ulionekana vizuri kwa kuwa nywele zilikuwa zimelowa maji. Kwa miaka mingi Naomi amekuwa akionekana na nywele za bandia, hivyo kitendo cha kuonekana hivyo kiliwashangaza wengi.
Naomi Campbell
Naomi Campbell

No comments:

Post a Comment