Monday, August 13, 2012

WEMA: HUYO WEMA WA FACEBOOK NI TAPELI


 

STAA wa filamu nchini, Wema Sepetu ameamua kufunguka kwa kusema kuwa anakerwa na watu wanaotumia jina lake katika mitandao mbalimbali ya kijamii ukiwemo wa Facebook, kwani wanamuharibia mambo yake mengi.
Wema ameliambia gazeti hili kuwa ana zaidi ya miezi 12 tangu alipojitoa kwenye mtandao wa Facebook, lakini bado kuna mtu anatumia jina lake vibaya kwa kuomba fedha kwa watu jambo ambalo linamkera kupita kiasi kwani amekuwa akipigiwa simu na watu wakimuuliza kulikoni.
“Yaani nakerwa sana na watu wanaotumia jina langu kutapeli au kuomba fedha kwenye mtandao, halafu nawaomba wale waandishi wa blog wanaoandika stori zao na kudai wamezungumza na mimi kumbe siyo kweli, waache upuuzi huo.
“Mashabiki wangu wakiona mtu anatumia jina langu kwenye Facebook wajue huyo ni tapeli na siyo mimi,” alisema Wema.

No comments:

Post a Comment