Friday, September 14, 2012

JUMA NATURE ADAIWA KUMTELEKEZA MWANAE


                                                                 JUMA NATURE
Mtoto wa Juma Nature
Hitmaker wa ‘Hili Game’ Juma Kassim Nature huenda akajikuta matatani hivi karibuni na ustawi wa jamii baada ya kumkataa mtoto anayedai msanii huyo ni baba yake mzazi.

Mtoto huyo mwenye miaka 17 aitwaye Samson Juma Kassim Kiroboto ameamua kusafiri kutoka mkoani Morogoro hadi Dar es Salaam ili kumfuata baba yake.

Samson aliyelazimika kwenye Clouds FM kutafuta msaada wa jinsi ya kumpata baba yake huyo, amesema mama yake alishafariki hivyo anamhitaji baba yake ili maisha yaendeleee.

Hata hivyo katika jitihada za kumtafuta Juma Nature, Samson amesema aliwawahi kwenda kwa bibi yake Temeke (mama yake na Nature) lakini alifukuzwa kama paka mwizi na bibi yake aliyemwambia hataki kumuona tena.

No comments:

Post a Comment