Monday, September 17, 2012

MWANAMITINDO WA TANZANIA, FLAVIAN MATATA ASHIRIKISHWA KWENYE VIDEO YA LADY GAGAMwamitindo wa kimataifa wa Tanzania na Miss Universe Flaviana Matata jana amepost picha akiwa na Lady Gaga ambaye hata hivyo sura yake haionekani vizuri kwakuwa anaonekana usoni akiwa amevaa maua yaliyozungushwa kwenye duara.

Miongoni mwa picha hiyo, kuna picha ambayo anaonekana msanii huyo wa ‘Born This Way’ akimbusu Flaviana Matata.
Katika picha hiyo Flaviana ameandika maneno aliyomnukuu Lady Gaga aliyomwambia “thank you for doing my video gal,u killed it”.

Kwa maelezo hayo inaashiria kuwa Flaviana ataonekana kwenye video ya msanii huyo mwenye vituko kibao.
Flaviana Matata yupo mjini London, Uingereza kwenye tamasha la London fashion week.

Naye Lada Gaga yupo London kwaajili ya uzinduzi wa perfume yake, FAME ambapo imedaiwa ametumia paundi milioni 1 kwenye uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment