Monday, October 1, 2012

MDOMO WAMPONZA JACKLINE WOLPER NA KUYAFANYA MAISHA YAKE YAWE YA CHUMBANI

 
 
 
SIKU chache baada ya mwigizaji Jacqueline Wolper Masawe kumlipua mchumba’ke, Abdallah Mtoro, ‘Dallas’ inadaiwa kuwa mwigizaji huyo anaishi kwa ‘machale’ akihofia kuuawa kutokana na ukweli wa maisha yao aliouanika gazetini.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, Dallas hakufurahishwa na sentensi za Wolper ambazo alizielekeza kwake huku akidai amemdhalilisha aliposema kuwa jamaa huyo hana chake na anatembea na nguo zake katika gari ili muda wowote amkabidhi.

“Kusema kweli sasa hivi Wolper anaishi kama digidigi, haonekani hovyo kama zamani.Nadhani anamuogopa mpenzi wake maana huenda akamfanyia kitu mbaya". kilisema chanzo chetu na kuongeza.

"Kauli alizozitoa gazetini zilikuwa tata sana na huenda zimemuuma sana mchumba wake ambaye alikuwa nimtu wake wa siku nyingi"

No comments:

Post a Comment