Tuesday, November 6, 2012

BABY MADAHA AJIUNGA NA KUNDI LA "TMK WANAUME HALISI"
MSANII wa muziki na filamu Baby Madahaameuambia mtandao huu kuwa kwa muda mrefu amekuwa akitamani kufanya kazi na kundi la muziki kutoka Temeke, TMK Wanaume Halisi, hivi sasa tayari ameshajiunga na kundi hilo na anadaii atafanya muziki wake kwa moyo mmoja kwani kundi hilo halina ubabaishaji kama yale mengine aliyotaka kujiunga nayo awali.
Mwandishi wetu alimtafuta msanii huyo kuzungumzia track aliyoshirikishwa na Juma Nature inachokwenda kwa jina la‘Narudi Kijijini’, ambapo alidai kuwa huo ni ukurasa mpya alioufungua na kundi hilo na sasa amejiunga kufanya ngoma nyingine kibao akiwa na wakali hao.

“Nimejiunga TMK Wanaume Halisi kwa sababu nawajua hawa ni wasanii ambao wanafanya kazi na si wale ambao wanakuwa na majungu majungu kwenye kazi nina imani kuwepo hapa nitafanya muziki vizuri kwani Juma Nature amekuwa akinipa ushauri sana juu ya muziki, hivyo mashabiki wangu wategemee mambo mazuri kutoka kwangu,” alisema.

No comments:

Post a Comment