Wednesday, June 27, 2012

KOVA AZUNGUMZIA UTEKAJI WA DK. STEVEN ULIMBOKA

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.

Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
Waandishi wa habari waimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Dk Steven Ulimboka akiwa amejruhiwa vibaya na watu wasiojulikana baada ya kutekwa na kupigwa vibaya usiku wa kuamkia leo na kuokotwa huko Mabwepande.
chanzo: Full Shangwe

No comments:

Post a Comment