Saturday, June 16, 2012

Ney Wa Mitego: Nimepiga Roba Sana ZamaniMsanii wa hip hop nchini Tanzania Ney wa Mitego amesema amepitia mengi mpaka alipo sasa na kuna wakati alikuwa akikaba watu njiani ili kujipatia riziki.
Katika mahojiano na East Afriica Radio jana, Ney anayefahamika kwa tabia yake ya kudiss wasanii wenzake, amesema tabia chafu na ujeuri vilimfanya afukuzwe nyumbani kwao wakati akiwa darasa la saba.
Katika kile kilichoonekana kama kupotea, Ney aliamua kuwa mkabaji wa usiku jambo lililomfanya mama yake amsuse.
Katika hatua nyingine msanii huyo amesema aliandika wimbo uitwao ‘Mwanamke hapigwi’ kutokana na uzoefu aliouona kwa mama yake mzazi.
Ameeleza kuwa nyumbani alikuwa akiishi na baba wa kambo ambaye mara nyingi alikuwa akimpiga sana mama yake kiasi cha kumfanya ashindwe kujizuia kuingilia.
Hata hivyo amesema kila alipokuwa akifanya hivyo mama yake alichukia na kuwa upande wa mpenzi wake huyo jambo lililomfanya aondoke kabisa kwao.
Hata hivyo inaonekana kuwa kwa sasa yeye na mama yake wana uhusiano mzuri baada ya kusema hewani kuwa anampenda sana.
Kuhusu tabia yake ya kudiss wasanii wenzie, Ney amesema hiyo ndio asili yake tangu kitambo na ukimzingua, anakuchana.
Hivi karibuni amemdiss Chidi Benz kwa kitendo chake cha kutoboa pua na kuuliza kuwa ‘labda mwenzetu sio riziki (Shoga). Hata hivyo baada ya Chidi Benz kuulizwa kuhusiana na suala hilo alidai kuwa hamjui Ney wa Mitego na hajawahi kumsikia.

chanzo:bongo5
 

No comments:

Post a Comment