Monday, June 18, 2012

WOLPER ANYANG’ANYWA GARI!!


Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.
Habari zenye ukweli 100% ambazo  zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.
Aidha chanzo hicho, kimeieleza kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana zoezi la kumsaka Wolper likakamilika, baada ya kuulizwa aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.
Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisme hivi: “Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa.  
                            Chanzo:teentz.com

No comments:

Post a Comment