Sababu ya kifo cha Josephine Okoye,mama wa nyota wa muziki wa R & B nchini Nigeria wa kundi la Psquare, Peter na Paul imejulikana.
Maelezo ya msemaji wa Psquare yamesema mama yao alifariki saa chache baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo nchini India.
Mrs.Okoye alipelekwa nchini India kwaajili ya kufanyiwa operation baada ya kukaa katika hospitali ya St.Nicholas ya nchini Nigeria kwa muda, ambayo ni miongoni mwa hospitali ghali nchini humo.
Wakati huo huo, watu maarufu wamekuwa wakimimika kwenye nyumba ya kifahari ya P-Square iitwayo Square Ville, kuungana na ndugu na jamaa kwenye msiba huo.

Pamoja na watoto wanne aliokuwa nao, Mrs Okoye ameacha mjukuu mmoja kutoka kwa Peter Okoye aliyezaa na Lola Omotayo