Monday, August 13, 2012

MUZIKI MGUMU, BWANA MISOSI AKIMBILIA FILAMU


SANAA ya muziki kwa sasa imekuwa na ushindani mkubwa, hali hiyo imesababisha wakongwe kadhaa kuelekeza nguvu kwenye kazi nyingine au kujiweka pembeni kabisa kwa kuwa ushindani ni mkubwa na hata vijana wanaochipukia nao wamekuwa na kasi kubwa.
Staa wa kitambo wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Lushalu ‘Bwana Misosi’, naye ameingia kwenye orodha ya wakongwe ambao wameamua kuelekeza nguvu kwenye kazi nyingine, baada ya kuamua kujikita kwenye uigizaji wa filamu.
Bwana Misosi alifumwa  akiwa mzigoni kwenye Kampuni ya Chuz Entertainment, maeneo ya Mwananyamala jijini Dar.
Alipoulizwa kulikoni, alisema: “Najua mkurugenzi wa kampuni hii (Tuesday Kihangala) atanisaidia kukuza kipaji cha uigizaji. Nawaomba mashabiki wasubiri kazi zangu lakini kwenye muziki napo sijaacha, nitaendelea kutoa nyimbo kama kawaida.”

No comments:

Post a Comment