Monday, August 20, 2012

RAY C ATUA BONGO, ASAKA MUME!

Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MSANII ‘first class’ wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amerejea Bongo na kutangaza kusaka mume huku akiweka wazi vigezo anavyotaka awe navyo, Jelard Lucas anashuka nayo.Akichonga na Over The Weekend juzikati, Ray C aliyekuwa amejichimbia nchini Kenya, alisema mwanaume atakayeweza kupata penzi lake anatakiwa kuwa na elimu ya kawaida, maendeleo, asiwe mwanamuziki wala pedeshee, awe na mvuto na mwenye kuyajua vizuri malavidavi.Mwanadada huyo ‘chakaramu’ aliongeza kuwa mwenye sifa hizo akipatikana, atamzalia watoto wawili na kujenga naye familia bora kwani amechoshwa na maisha ya usela.“Sina mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.Kuhusu kurudi kwenye gemu, Ray C aliwaahidi mashabiki zake kuwa baada ya mfungo kumalizika, yupo kwenye harakati za kuzindua albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Moyo Waniuma’ yenye nyimbo 10.
Aliongeza kuwa soko la muziki Bongo ni bovu sana ukilinganisha na Kenya hivyo bado mishemishe zake nyingi atakuwa akizifanyia nchini humo

No comments:

Post a Comment