Friday, September 7, 2012

AIRTEL YAMTANGAZA AY KUWA BALOZI

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kati) akimtangaza msanii Ambwene Yessayah (AY) (shoto) kuwa Balozi wa Airtel Tanzania kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania kwa mwaka 2012 -2013, AY sasa atashirikiana na Airtel katika shughuli zote za kijamii za Airtel nchini kwa lengo la kufaidisha taifa letu hasa sekta ya ELIMU. Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (shoto) akimkabidhi msanii Ambwene Yessayah (AY) simu aina ya Sumsung Galaxy mara baada ya kumtangaza AY kuwa Balozi wa Airtel kwa Upande wa wasanii nchini Tanzania, AY sasa kushiriki shughuli zote za kijamii za Airtel nchini. Kulia ni Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu za Airtel jijini Dar es Salaam.

 
Dar es salaam 06 September 2012, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imemtangaza Balozi wake mpya kwa mwaka 2012-2013 ikiwa ni utaratibu iliyojiwekea katika kushirikiana na wasanii nchini ili kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
AY ni msanii mahiri nchini kwenye muziki wa kizazi kipya aliyejipatia heshima na kuvuta hisia za wapenda burudani wengi pale anapokuwa jukwaani, AY alijulikana zaidi baada ya kuachia album yake ya kwanza iliyobeba wimbo mkali wa ‘Raha kamili” na kufanya apendwe zaidi kitaifa na kimataifa kuanzia mwaka 200.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeingia makubaliano na msanii AY kuwa Balozi wetu wa mwaka huu, lengo letu ni kuendelea kuwa karibu zaidi na wasanii wetu nchini na pia kufanya nao shughuli za kijamii ili kufaidisha taifa letu kwa kuwa wasanii wetu ni mahiri zaidi na wote tunafahamu AY ni msanii mkongwe na anayejituma, hivyo tunaamini ushirikiano huu utaweza kutimiza malengo yetu ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kuhudumia jamii kupitia miradi mbali mbali ya jamii inayoendeshwa na Airtel pamoja na kuiwakilisha Airtel kwa kuwa Balozi mzuri.
“Sasa AY atakuwa ni msanii wa pili kuingia mkataba kama huu ambapo mwaka uliopita alikuwa Ali Kiba. Tulimtangaza Ali kiba kuwa Balozi wa Airtel mwaka jana na ameshirikiana na Airtel kikamilifu katika shughuli mbalimbali za kuitangaza Airtel kupitia matangazo ya radio, Luninga, Mabango na Mabandiko lakini pia alifanikiwa kuiwakilisha nchi yetu kwenye wimbo wa Hands Across the World alioimba na wasanii wengine wa kimataifa akiwemo R. Kelly katika kundi la One8 kwa udhamini wa Airtel na kufaulu sana kubainisha umahiri wa wasanii wa Tanzania kwenye mataifa mengine makubwa kupitia kazi yake nzuri aliyofanya ndani ya wimbo huo”aliongeza Mmbando.
AY ni msanii mwenye umahiri wa hali ya juu pale anapokuwa jukwaani, AY ameshafanikiwa kufanya matamasha ya kimataifa huko USA, UK, Spain, Dubai, Burundi, Rwanda, Ethiopoa, Malysia, India, Russia, Afrika ya kusini, Kenya na Uganda ikiwa ni pamoja na kufanya nyimbo nyingi na wasanii wengi wa kitaifa na kimataifa.
Wasanii waliowahi kufanya nyimbo na AY ni pamoja na Chameleon, Ngoni (Uganda) , Amani, Nameless, Jua Cali (Kenya), P.Square, J.Martins (Nigeria) wengine ni msanii wa kimataifa Ms.Trinity, Sean Kingston anayewika Jamaica pamoja na Lil Romeo wa USA.
Vilevile AY ni msanii wa kwanza wa kiume nchini Tanzania kutunukiwa tuzo ya KORA mwaka 2005, na kupata pia tuzo ya MTV MAMAs ya 2009 pamoja na kutunikiwa France Awards mwaka 2010. Na hivi sasa amechaguliwa katika kuwania tuzo za Channel O katika vipengele vitatu; Video bora ya Africa, Video bora ya mwaka na mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka.
Kwa upande wake Ambwene Yessayah kama balozi wa Airtel alisema “kwa kushirikiana na Airtel nitakuwa nikifanya shughuli za kijamii, hususani katika kuchangia ukuaji wa Elimu nchini. Pamoja na Airtel tutashirikisha vyombo na taasis nyingine ikiwemo vyombo mbalimbali vya Habari ili kuweza kufanikisha yote hayo. Kwa Kushirikiana na Airtel tutaandaa maonyesho mbalimbali ya burudani kwa ajili ya wateja wetu na hii itatangazwa hivi karibuni”.
“Na kwa kuanza kama balozi wa Airtel napenda kuwaomba na kuwaimiza Watazania wenzangu kuweza kuchangia mradi ambao tumeshauanzisha wiki tatu zilizopita tukishirikiana na BAMVITA katika kuchangia vitabu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum. Kampeni hii ya ushirika na Bamvita itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu, na Watanzania tunaweza kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na kwakufanya hivyo kila SMS tutakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200 itakayoingizwa yote katika mradi huu.”
“Vile vile wadau wengine wote wataweza kuchangia kwa kupitia huduma ya Airtel Money ambapo jina la fumbo ni VITABU au kutuma michango yao kwenda namba 0788041361. Hivyo basi ningependa kuwahamasisha watanzania wote kuchangia kiasi chochote mtakachoweza pia unaweza kuchangia zaidi ya mara moja.”

No comments:

Post a Comment