Friday, September 14, 2012

IKULU:Taswira mbalimbali za Ziara rasmi ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Kenya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais jakaya kikwete akiweka shada la maua kwenye kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Mama Salma Kikwete akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho
Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho
Rais Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja n ujumbe wake na wanachuo na viongozi wa chuo hicho baada ya kukitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment