Monday, September 24, 2012

IRENE UWOYA APATA SHAVU LA KUFANYA FILAMU MOJA NA NYOTA WA MAREKANI ‘HALLE BERRY

 

 
 
WAKATI msanii Irene Uwoya akiendelea kufanya mchakato wa kutaka kushiriki kwenye filamu za kimataifa, tayari inadaiwa kuwa anatarajia kula shavu kubwa ambalo hajawahi kuliota la kushiriki filamu moja na msanii maarufu Halle Berry kutoka marekani.

Halle Berry
ni moja ya wasanii mahiri kabisa ambao wana uwezo mkubwa kwani ameweza kuonesha uwezo wake kwenye filamu kama ‘Die Another Day’, Catwoman, New Year’s Eve, Monster’s Ball na nyingine nyingi.

Ishu ya
Uwoya kushiriki ndani ya filamu moja na mwanadada huyo inadaiwa kuwa katika mazungumzo anayofanya nchini Uingereza mmoja ya wadau wakubwa ya tasnia hiyo kutoka Marekani ndiye aliyempa ishu hiyo baada ya kuona baadhi ya filamu alizocheza pamoja kujiamini kwake.

Uwoya alidai kuwa bado hajaamini kwani hajapewa ishu kamili na ameambiwa kuwa atajulishwa kwa njia ya email endapo kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu ya ratiba ya Berry.


“Naweza kucheza filamu moja na Halle Berry, ingawa sijajua kama ishu hii inaweza kuwa kweli kwa sababu kama unavyojua kila kitu huwa kinaenda kwa ratiba siyo kama sisi bongo filamu tunajitolea bila hata kufuata ratiba,”
a
lidai
 

No comments:

Post a Comment