Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na
Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya
kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo
kama Food, Agriculture and Natural
Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.
Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo
hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera
bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi
Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa
mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati
Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa kufuata njia
za kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo,
leo Septemba 6, 2012
No comments:
Post a Comment