Tuesday, September 11, 2012

SIMBA YASHINDA NGAO YA HISANI, YAIKUNG’UTA AZAM FC MAGOLI 3-2 U/TAIFA

Nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma akinyanyua juu ngao yao ya hisani baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi katika mchezo wa kukaribisha Ligi Kuu ya Tanzania bara .
Timu ya Simba imefanikiwa kushinda ngao ya hisani kwa kuifunga timu ya Azam FC magoli 3-2 yaliyofungwa na Daniel Akufo, Mwinyi Kazimoto na Emmanuel Okwi, wakati wachezaji wa Azam FC Kipre Cheche pamoja na John Boko wamefunga magoli kwa upande wa Azam FC goli la kwanza la Simba limefungwa na kwa penati, baada ya wachezaji wa Azam kuunawa mpira katika eneo la hatari wakati wakimzuia mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi aliyekuwa akielekea golini kwao


Nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma akipokea ngao ya hisani kutoka kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na ajira Mh. Makongoro Mahanga huku wachezaji wa timu hiyo wakishuhudia.Mshabuliaji wa timu ya Simba Daniel Akufo akijaribu kuwatoka beki wa timu ya Azam FC Agrey Morris na golikipa wa timu hiyo Deo Munishi wakati wa mchezo wa ngao ya hisani kama uzinduzi rasmi wa ligi kuu ya Tanzania bara inayotarajiwa kuanza jumamosi Septemba 15.


Beki wa pemben i Nasoro Cholo wa Simba katikati akijaribu kupenya na kuwatoka Golikipa wa timu ya Azam FC Deo Munishi na Beki wa timu hiyo Agrey Morris katika mchezo wa ngao ya hisani kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.


Wachezaji wa Simba wakitoka nje baada ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.


Mashabiki wa timu ya Simba wakizomea wenzao wa timu ya Azam FC hawapo pichani.

Washabiki wa timu ya Azam FC wakiwakejeli wenzao wa Simba hawapo pichani baada ya kuwatangulia kwa magoli 2-1 katika mchezo wa ngao ya hisani uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment