Friday, October 5, 2012

CHRIS BROWN AMPIGA CHINI MPENZI WAKE KISA KIKIWA NI RIHANNA

 

Chris Brown amesema ameachana rasmi na mpenzi wake Karrueche Tran … kwa maelezo kuwa hapendi kumuona akiumia kutokana na urafiki wake na Rihanna.

Brown ametoa taarifa hiyo kwa kusema “Nimeamua kuwa single ili kufocus kwenye kazi yangu. Nampenda sana Karrueche lakini sipendi kumuona akiumia kwasababu ya urafiki wangu na Rihanna.


Ameongeza,”Ni afadhali niwe single ili sote tuwe na furaha na maisha yetu.”

Tangazo hilo la Chris Brown limekuja baada ya Brown na Rihanna kuonekana pamoja kwenye show ya Jay Z huko Brooklyn juzi usiku.

Hata hivyo Karrueche amedaiwa kutoiamini kauli ya Chris kuwa ni rafiki tu na Rihanna na amewaambia marafiki zake kuwa anaamini wawili hao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Mtandao wa TMZ umesema kuwa Karrueche anaona amesalitiwa na mpenzi wake huyo kwakuwa alimwahidi kuwa yeye ndio mwanamke pekee katika maisha yake baada ya kutaka kujua msimamo wake juu ya Rihanna.

Umesema Karrueche alikuwa ameshachezwa ‘machale’ kuwa wapenzi hao wa zamani walikuwa wakimzunguka kwakuwa wiki mbili zilizopita Chris alikuwa amebadilika kwa kwenda klabu peke yake na kumkwepa mpenzi wake.


Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa Karrueche aliwaambia marafiki zake kuwa alimpenda Chris kwa dhati na alihisi uhusiano ulikuwa imara mpaka pale Rihanna aliporudi tena kwenye picha.

No comments:

Post a Comment