Wednesday, October 10, 2012

LINEX ASHITAKIWA KWA KUMPIGA KOFI LA KWELI MREMBO ALIYECHEZA NAYE VIDEO YA AIFOLA!!!!

 
Hiki kinaweza kuwa kituko cha mwaka kwenye muziki wa Bongo Flava. Mrembo aliyeigiza kwenye video ya Linex Aifola, ameamua kumfungulia RB msanii huyo baada ya kumpiga kibao cha kweli kwenye video hiyo.

Katika video hiyo Linex anaonekana akiwa amekaa kwenye kochi na kuanza kukagua simu ya mchumba wake Aifola ambaye humo ameigiza Janeth Bundala na ndipo alipogundua kuna meseji za kimapenzi anazotumiwa na mwanaume mwingine kiasi cha kuchukia na kumpiga kofi kali la shavuni.


 
“hahhahahahhahaha frm no where eti janeti aka aifola kanipigia leo kaniambia kanichukulia R B kwa kofi nililompiga wakati tunaigiza hahah kama kachelewa hv,” aliandika Linex jana kupitia Facebook.
“Sijajua alikua anatania but ndo kitu alichoniambia muda si mrefu nimekia nacheka tu. Nimemsikia live radion anataka kulipwa aseeee kumbe anamaanisha. Nimeshaongea nae na kesho ndo nakutana nae rasmi ntajua anatakaje na ntamalizana nae.”

Unahisi Janeth yuko sahihi kumshtaki Linex kwa kumpiga kibao cha kweli kwenye uigizaji wa video? Na je amechelewa kama Linex anavyosema?

1 comment: