Wednesday, October 31, 2012

WAKAZI WA DAR WAFURAHIA USAFIRI WA GARI MOSHI


Bi. Rose Ngauga akizungumza  na mwandishi wetu aliyemtembea ofisini kwake kujua mawili matatu kuhusiana na usafiri huo.
WAKAZI wa Jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake, wamefurahia kuanza kwa usafiri wa treni waliousubiri kwa muda mrefu ulioanza juzi.
Abiria wakigombea kupanda treni kutoka katikati ya jiji kueleke Ubungo.
Kamera yetu leo ilitua katika ofisi ya mkuu wa kituo kinachodili na usafiri huo, Bi. Rose Ngauga na kuzungumza mambo kadhaa kuhusiana na usafiri huo.Ngauga alisema kuwa usafiri huo siyo nguvu ya soda kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na kwamba utakuwa endelevu.

3. ….akimuonyesha  mwandishi wetu tiketi zinazotumika  kwa abiria wa kawaida  na wanafunzi.

4. Abiria wakiwa katika dirisha la kukatia tiketi.

5. Wanafunzi wakikata tiketi katika dirisha maalumu kwa ajili yao.

6. Kichwa cha treni kikiunganishwa na mabehewa kabla ya kuanza safari.

8. Abiria wakiwa wameketi ndani ya behewa wakisubiri kuanza safari.

9. Mkuu wa Kituo cha Reli, Bi. Rose Ngauga akikagua mabehewa kabla ya gari moshi kuanza safari leo saa 9.40 alasiri.
10…. akikabidhiwa ripoti.
11.Wanafunzi wakipanda katika behewa lao maalumu tayari kwa safari.
12. Gari moshi likiwa katika mwendo na baadhi ya abiria wakionekana wakichati na simu.
13. Mwandishi mwanadamizi wa Global Publisher, Haruni Sanchawa  akishuka kutoka katika treni hiyo  maeneo ya Ubungo Maziwa ambako treni hiyo umalizia safari yake.
14. Abiria wakishuka kwenye treni.
15. Pamoja na usafiri huo kuanza, mafundi wa shirika la reli bado wanaendelea na ukarabati  wa reli kama wanavyoonekana pichani.

(HABARI PICHA : Haruni Sanchawa / GPL )

No comments:

Post a Comment