Thursday, August 16, 2012

BELINA ALA SHAVU NONO....HIVI SASA NI BALOZIMwanamitindo Belina Mgeni.


MWANAMITINDO mwenye mvuto Bongo, Belina Mgeni amelamba shavu la nguvu kutoka kwa kampuni kubwa ya nywele nchini kwa kusainishwa mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa kampuni hiyo.‘Akisemezana’ na waandishi wetu, Belina alisema anamshukuru Mungu kwa kupata shavu hilo ambapo sasa picha zake zitakuwa zikionekana katika mabango ya kampuni hiyo, pia atakuwa akisuka bure nywele kwa kipindi cha mwaka mmoja na kutumia bidhaa za kampuni hiyo kama balozi.


Aidha, mwanamitindo huyo alisema ataubeba ubalozi huo kwa umakini mkubwa kwa sababu heshima waliyompa ni kubwa sana kwa upande wa warembo na wanamitindo wa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment