Monday, November 26, 2012

MSANII AFARIKI GHAFLA !!!!
MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa akipanda juu kwa kasi, John Maganga (22) amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokimbizwa akiwa hoi, inasikitisha sana.

John Maganga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baba mdogo wa John, Deogratius Shija alisema Ijumaa iliyopita, marehemu alipatwa na maumivu ya ghafla ya tumbo, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu ya Mwananyamala, Dar ambako vipimo vilidai utumbo wa mgonjwa huyo ulitoboka.
Shija: “Daktari akatuambia kutokana na hali hiyo watamfanyia upasuaji ili kuuziba utumbo huo lakini mara baada ya zoezi hilo daktari akasema tatizo halikuwa kutoboka kwa utumbo bali kuna kitu kingine. 
“Ikabidi tumkimbize Muhimbili ambako madaktari wa pale walituambia wenzao wa Mwananyamala walikosea kumfanyia upasuaji John kwani tatizo halikuwa la kufanyiwa upasuaji bali alitakiwa apatiwe dawa.
“Madaktari wakatuambia tumwache pale ili waokoe maisha yake sisi ndugu turudi asubuhi. Tulipokwenda asubuhi tukaambiwa mgonjwa wetu alifariki dunia usiku uleule. Imetuuma sana.”      


Hivi karibuni, John aliandaa filamu yake ambayo aliipa jina la Beautfools ambayo yeye alicheza kama mume wa ndoa wa Aunt Ezekiel ambaye alimtenda John wakati anasoma chuo.
Marehemu alikuwa akienda vizuri katika tasnia ya filamu na ilisadikiwa angeweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. Kifo cha John kimeacha pigo kubwa Bongo Movies ambayo mpaka leo vilio vimetawala.
Mpaka jana Jumamosi, mazishi ya msanii huyo yalikuwa yakimsubiri mama yake mzazi aishie London Uingereza.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina

No comments:

Post a Comment