Tuesday, November 27, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA....!!!!! 

Habari zenye uhakika na zilizothibitishwa ni kwamba sharo milionea amefariki dunia leo hii usiku wa saa 2 kwa ajali ya gari huko MAGUZONI tanga na maiti iko katika hospital ya teule muheza, kwa habari za alieshuhudia ajali kulwa mbondei amesema marehemu alikuwa peke yake katika  ajali hiyo na alikuwa na gari aina ya HARRIER,Alisema gari iliacha njia na kuingia mapolini na kugonga mti baada ya hapo ilibingirika bingirika zaidi ya mara tatu na kupelekea kifo chake marahemu ameumia sana maeneo ya kichwani na jichoni .hapo ndipo wasamalia wema walipochukua simu yake nakuangalia majina ya watu kwenye simu nakumpigia simu TUNDA MAN kwamba sharo milionea amepata ajali na amefariki maiti ipo hospital ya teule muweza.hapo ndipo taaarifa za kifo cha sharo zilipoanza kusambaa. mungu mlaze mahala pema peponi SHARO MILIONEA


No comments:

Post a Comment