Saturday, November 3, 2012

Ndikumana: NimerogwaStori: Musa MatejaMUME wa mcheza filamu za Kibongo, Irene Uwoya, raia Rwanda, msakata kabumbu wa Klabu ya Rayon ya nchini humo, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ amepasua jipu na kusema kuwa, amepigwa ndumba nchini Tanzania na mwanamke ambaye hataki kumtaja kwa sasa.
kitu ambacho kinasadikiwa kuwa amelishwa
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu kutoka Rwanda, Kataut alisema kuwa amelazimika kuweka wazi madai  hayo ili aliyemfanyia kitendo hicho aweze kutambua kuwa ameshajua na lengo lake la kumteketeza  halitafanikiwa tena.
 Hamad Ndikumana ‘Kataut’ akiwa na Irene Uwoya enzi za mapenzi yao
Kataut ambaye alitua Rayon baada ya kuachana na soka la kulipwa nchini Cyprus,  amemwambia mwandishi wetu kuwa mwanamke aliyemfanyia uchawi huo ni Mtanzania na ni mweupe ‘pee’  ambaye alikuwa na lengo la kumuua.
 Msakata kabumbu huyo alisema kuwa, ametolewa vitu vya ajabu mwilini mwake na mganga wa kienyeji baada ya kusumbuliwa na maradhi  kwa takribani  mwaka mmoja na kumfanya azunguke nchi mbalimbali kutafuta matibabu.
Irene Uwoya
“Nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa mwaka sasa na kila nilipoenda hospitali ugonjwa ulikuwa hauonekani, hadi nilipopata tiba za asili, leo hii nimepata nafuu baada ya kuzunguka kwa waganga saba wa kienyeji,” alianza kwa kusema Ndikumana.
Ndikumana aliyemuoa Uwoya mwaka 2008 na kufanikiwa kupata naye mtoto mmoja aitwaye, Dagrei Krish alisema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua ni ule wa kuwashwa sehemu za siri  huku akisikia maumivu makali jambo ambalo wakati mwingine lilimfanya kujikuna na kutoka vidonda vikubwa ambavyo havikupona pamoja na kupewa dawa tofauti.
“Najua ni vigumu mtu kuamini ninachokisema kwa kuwa watu hawayajui maumivu niliyokuwa nikiyapata, hivyo ukweli utaendelea kubaki ndani ya nafsi yangu na sasa nimeamini kwamba kuna watu wengi huwa wanachezewa kwa ushirikina,” alisema.
Katika kuhangaika kutafuta tiba, Ndikumana ambaye alitengana na Uwoya  katika mazingira ya kutatanisha mwaka jana,  alisema kuwa Agosti mwaka huu alifika Tanzania na kukaa siku mbili kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa ugonjwa wake.
“Nilielekezwa Arusha ambako hata hivyo mambo  hayakuwa mazuri, nikaamua kurudi Kigali nilikofanikiwa kutibiwa,” aliongeza.
Kataut alisema kuwa kabla ya kupona, Septemba mwaka huu alitembelea nchi mbalimbali kusaka tiba na kumfanya kufika hadi Jahmhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) kote huko alikuwa  akitajiwa jina  la mtu aliyemfanyia ubaya huo.

“Namshukuru Mungu kwa kuwa nimepona, baada ya kutolewa kitu mwilini mwangu, hivyo aliyenifanyia mchezo huu ajue dhamira yake ya kuniua imeshindikana, ni vyema akajua kuwa amekwama na nitakuja kumtaja hadharani ili kila mtu amfahamu,” alisema  Ndikumana.

No comments:

Post a Comment