Sunday, May 20, 2012

MIRIAM ODEMBA AMTESA KIM KARDASHIAN

Miriam akiwa katika pozi
NANI alijua kuwa hata wanawake wazuri kama Kim Kardashian nao huwa wanateswa na wivu, basi amini usiamini Miriam Odemba alimnyima raha mlimbwende huyo baada ya kuwa bega kwa bega na 'boy frend' wake, Kanye West.
Inadaiwa kuwa Kim alianzisha patashika nyuma ya jukwaa wakati mpenzi wake huyo akizindua nguo zake mpya huko Ufaransa.
Kim na Kanye walikuwa Paris kwa shughuli hiyo na Odemba yuko huko Ufaransa kwa kazi yake ya kuonyesha mavazi.
Inasemekana Odemba aliwahi kukutana na Kanye West na kujuana mwaka jana wakati rapa huyo akizindua nguo za kwanza huko Ufaransa.

Sasa wikiendi hii Kanye West alipokwenda tena Odemba baada ya kumuona rafiki yake, alimchangamkia na kujumuika naye kucheza muziki kitendo ambacho hakikumfurahisha Kim.
Wakati Kanye akicheza na Odemba, Kim alikuwa amekaa na Swizz Beatz na mkewe Alicia Keys, unaambiwa Kim alikuwa hapepesi macho kwa wivu.
Hata hivyo Kim anadaiwa kuwa alishindwa kuendelea kuvumilia kuona mwanamke mrembo akiendelea kucheza na mpenzi wake na kuhatarisha penzi lao changa. Moja kwa moja alimvuta Kanye huku maneno yakimtoka.
Mastaa wengine waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na
D’Banj, P.Diddy, common, Big Sean, Cassie na Waka Flocka Flame.
Kanye West

1 comment:

  1. Mmmh kwenye mapenzi hakuna uzuri babu wee,nimependa kim alivoact kwani ameshow her feelings to kanye

    ReplyDelete