Habari
zilizopatikana hospitalini hapo, zinaeleza kuwa, mtoto huyo alizaliwa
usiku wa kuamkia jana akiwa na uzito wa kilo 3.5 na mwanamke mmoja
ambaye jina lake limekuwa siri.
Taarifa
hizo zilisema kuwa, mara baada ya mtoto huyo kuzaliwa, wakunga
waliokuwa wakimzalisha mwanamke huyo walishangaa kuona mtoto huyo akiwa
na vichwa viwili vilivyoungana katika kiwiliwili cha mwili mmoja.
Mmoja
wa wauguzi hospitalini hapo aliliambia NIPASHE kuwa, mtoto huyo mara
baada ya kuzaliwa alipelekwa haraka katika chumba maalum kwa ajili ya
uchunguzi.
“Kwa
kweli haijafahamika mara moja kama yule mtoto ana uwezo wa kunyonya ama
la, kwani wameungana shingoni wakati miguu na mikono ikiwa miwili
miwili,” alisema muuguzi huyo kwa sharti la kutotaja jina lake.
Hata
hivyo, mfanyakazi mwingine wa hospitali hiyo alisema juhudi zinafanywa
na madaktari bingwa wa hospitali hiyo kuchunguza kwa kutumia mashine
maalum kama vichwa hivyo vinachangia moyo mmoja.
“Madaktari
wapo katika harakati za kumfanyia uchunguzi kuangalia kama wanachangia
moyo kwa ajili ya kuangalia njia sahihi ya kuokoa maisha angalau ya
mtoto mmoja,” aliongeza.
Aidha,
habari kutoka ndani ya hospitali hiyo zinaeleza kuwa uongozi wa
hospitali umewazuia watu kwenda kumuona mtoto huyo baada ya kutokea
tukio la kuzirai kwa mmoja wa wanafamilia hiyo aliyekwenda kumuona.
Afisa
Uhusiano Msaidizi wa Muhimbili, Jezza Waziri, alipotakiwa kuzungumzia
suala hilo, alisema bado imekuwa mapema kuelezea tukio hilo kwa sababu
kuna hatua mbalimbali zinachukuliwa na uongozi wa hospitali hiyo kwa
ajili ya kulitolea ufafanuzi.
“Sina
la kuongea kuhusu tukio hilo, subiri kwanza tufanye mawasiliano na
viongozi wangu na kama ikihitajika kutolewa nitawaambia,” alisema
Waziri.
TUKIO KAMA HILI NCHINI
Matukio
kama hayo yamewahi kutokea nchini kwa mfano, mwanamke aliyejitambulisha
kwa jina la Devotha Ernesta, mkazi wa Msowero wilayani Kilosa, Mkoa wa
Morogoro, alijifungua watoto wa mapacha walioungana kuanzia sehemu ya
kichwa mpaka kiwiliwili wakiwa na miguu minne na mikono minne.
Tukio
hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu kwenye Hospitali ya Wilaya Kilosa,
baada ya mwanamke huyo kufika hospitalini hapo akiwa na ujauzito
uliokamilika siku za kujifungua.
Muda
ulipofika ndipo alipojifungua watototo walioungana wakiwa na uzito wa
kilo nne, lakini muda mfupi baada ya kuzaliwa walifariki dunia.
Mganga
Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Moses Mwemsanga, alisema kuzaliwa kwa
watoto hao ni hali ya kawaida inayoweza kutokea kwa mtu yeyote na kwamba
kunasababishwa na mbegu za kike na za kiume kuungana na baadaye
kushindwa kugawanyika.
Alisema
kuwa watoto hao walikuwa mapacha, lakini ilishindikana kugawanyika
baada ya mbegu za mwanamke na mwanaume kuungana na kuongeza kuwa ni hali
ya kawaida ambayo inaweza kutokea kwa mtu yeyote ingawa hutokea kwa
nadra sana.
Mwanamke
aliyejifungua watoto hao, Devotha Ernest, alisema katika maisha yake
hakuwahi kuona mtoto kama huyo aliyejifungua na hawezi kuhusisha na
imani za kishirikina bali ni mapenzi ya Mungu.
Devota
alisema alikuwa anatamani sana ajifungue salama apate furaha na mtoto
wake, lakini mwenyezi Mungu ameamua kutekeleza alichokusudia kwa mapenzi
yake na hawezi kuhusisha na tukio la kishirikina kutokana na
kujifungua mtoto huyo.
Tukio
la pili lilitokea Zanzibar Januari 1, 2010, ambapo mwanamke mkazi wa
mjini Zanzibar, Farihati Maulid (18), alijifungua watoto mapacha
walioungana.
Mwanamke huyo alijifungua kwa njia ya upasuaji katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Mapacha
hao walikuwa wa kiume ambao waliungana wakiwa na moyo mmoja na
waliunganika kuanzia kwenye kitovu hadi kwenye mfupa wa kidari huku
wakiwa na uzito wa kilo 2.8.
No comments:
Post a Comment