Monday, December 31, 2012

“SCENES ZA MAPENZI KWENYE FILAMU ZINAWAUMBUA WASANII WANAONUKA MIDOMO” – IRENE UWOYA

 


MSANII wa filamu anayejichukulia umaarufu bongo Irene Uwoya, amedai kuwa kuna baadhi ya wasanii wenye majina makubwa wanapenda kucheza filamu za mapenzi na uchezeana huku wakishindwa kuelewa kuwa wananuka midono na mara nyingine huwa wanavumulia pasipo kutoa ukweli huo.
Kauli kama ya msanii huyu iliwahi kutolewa na Janet Jackson kwenye filamu ya ‘Poetic Justice’ iliyozinduliwa mwaka 1993 akimtaka Tupac Shakur kupima  ukimwi kwani kuna kipande walitakiwa kuonekana wakipeana midomo kwani walicheza kama wapenzi ndani ya filamu hiyo, ndiyo kitu ambacho hata kwa wasanii wa kitanzania wanatakiwa kujifunza na si kukurupuka kupeana midomo..

Uwoya alisema kuwa kuna sehemu huwa wanakosea na kupeana midomo bila kupima afya kwani wapo wasanii wengine si wasafi na wananuka midomo huku wengine wakiwa wanatumia sana dawa za kulevya hivyo kuna hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa endapo wasipo chukua hatua.
Alisema kuwa wengine wanajijua walivyo lakini wanashindwa kujisafisha na kuwa katika hali nzuri badala yake ndani ya filamu wanaanza kupeanda kiss na kuchezeana bila kujua afya ziko vipi.

“Sasaivi naanza kuwa mkali kwa sababu endapo tukiendelea kuwa kimya tunaweza kujikuta magonjwa yanatukuta hivi hivi” aliongeza.
Hata hivyo msanii huyo aliwashauri baadhi ya wasanii wenye tabia za kupenda kupeana midomo ndani ya filamu wawe makini kwani huwezi jua ni ugonjwa gani anaoweza kupata, na kikubwa zaidi ni kupima kabla ya kazi kuanza ili kama kuna mtu mwenye tatizo apewe tiba mapema.

2 comments:

  1. nna video ya porn nmerekod chek me naiuza 0757303500

    ReplyDelete
  2. NAOMBA MFUTE HIYO COMMENT "nna video ya porn nmerekod chek me naiuza"
    0757303500 NIMEACHA HAYO MAMBO YA KISHETANI

    ReplyDelete