Thursday, July 26, 2012

ALIYEFANYA MAUAJI YA FAMILIA YA MWANAMUZIKI JENNIFER HUDSON,AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.

Mwaka 2008 ulikuwa mgumu kwa mwanamuziki wa nchini Marekani Jennifer Hudson.Tarehe 24 october alipoteza kaka yake,mama yake na mpwa wake ambao waliuwawa kwa kupigwa risasi.
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambae juzi alihukumiwa kifungo cha maisha anaitwa  William Belfour.Mtuhumiwa aliwahi kumuoa dada wa Jennifer anaeitwa Julia lakini walitengana kwa kutokuwa na maelewano mazuri.Katika ugomvi huo alimwambia ukiniacha mimi nitaiua familia yako yote halafu mwishoni nitakuua na wewe.
Mama wa mtuhumiwa akilia kwa uchungu baada ya mwanae kuhukumiwa kifungo cha maisha.
Jennifer akiwa na mama yake katikati ambae aliuwawa wakati dada mtu Julia mwenye nguo nyeupe akiwa ameondoka nyumbani kwenda kazini.Aliingia nyumbani na kumpiga risasi mama yao kwa nyuma mgongoni.
Na Kaka yake Jason Hudson aliuwawa kwa kupigwa  risasi  kichwani akiwa amelala kitandani.
Akaondoka na mtoto wa Julia anayeonekana pichani ambae mwili wake ulikuja kuonekana baada ya msako wa siku tatu.Alikutwa kwenye gari iliyotelekezwa akiwa amepigwa risasi kadhaaa kichwani.
Nyumba ya familia yake ikiwa imewekwa maua,misalaba na picha kama sehemu ya kumbukumbu ya mauaji ya familia hiyo.

No comments:

Post a Comment