Tuesday, July 10, 2012

MGOMO WA MADAKTARI ;MTOTO MGONJWA ARUDISHWA KWAO!!!



Daniel Mdogo Chemenzi akiwa na mwanae nje ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto Zawadi Daniel.
Na Makongoro Oging'
MTOTO Zawadi Daniel, 6, mkazi wa Kijiji cha Mautya, Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma amerudishwa kwao baada ya kukosa matibabu ya upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karabuni, baba mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Daniel Mdogo Chemenzi akiwa na huzuni huku machozi yakimtiririka alikua na haya ya kusema:
‘Nimetokea kijijini mkoani Dodoma na kumleta hapa Muhimbili kwa matibabu na ilibidi afanyiwe upasuaji kwani ana matatizo mengi kiafya likiwemo kichwa kujaa maji na kuwa kikubwa.
“Mara ya kwanza nilimleta Oktoba, mwaka jana kisha Februari, Mei na Juni 27, mwaka huu nilipofika wodini Muhimbili nilielezwa na wauguzi kuwa hakuna matibabu kutokana mgomo wa madaktari uliokuwa unaendelea, hivyo nitafute pa kumpeleka. (alifuta machozi).
“‘Niliposikia hivyo nilichoka sana niliamua kukaa chini huku nikiwaza ni jinsi gani nitafanya, hali ya mwanangu kiafya ilizidi kuwa mbaya sana hata kupumua kwake kulikua ni kwa shida.
“Sikujua pa kwenda kwa muda huo, sina ndugu hapa Dar es Salaam wala fedha kwa ajili ya kununua chakula wala kupangisha chumba cha kulala, ningekuwa na fedha kidogo ningempeleka hospitali ya binafsi ili akatibiwe.
“Nauli ya kuja Dar ilikua ya kuungaunga, yaani kuomba kwa watu ndiyo maana nimeamua kuja peke yangu bila kufuatana na mke wangu.”
Chemenzi alisema anarudi nyumbani kwake Dodoma bila kujua tarehe ya kurudi Muhimbili kwani hakukua na daktari wa kumpangia siku ya kurejea. Amewaomba wasamaria wema wamsaidie fedha kwa kutumia M-PESA kwa kutumia namba 0763 557098 wa kumuuguza mwanaye Zawadi.


Posted in global publishers

No comments:

Post a Comment