Tuesday, July 10, 2012

Mtoto alia baada ya kushindwa kuanza kidato cha kwanza


Na Haruni Sanchawa
MTOTO yatima Zainuli Hassan (16) (pichani) ambaye ni mwanafunzi aliyetakiwa kuanza kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mbopo iliyopo Madale jijini Dar es Salaam ameshindwa kuanza masomo yake.Kijana huyo amesema amekuwa akililia elimu lakini ameshindwa kuipata, anasimulia kwa masikitiko mbele ya mwandishi wetu kisa kilichosababisha asiende kusoma:
“Nilichaguliwa kuanza kusoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mbopo, Madale wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam lakini sijaripoti kwa sababu sina fedha za kulipia ada na vifaa vya masomo, ikiwemo sare na madaftari.
“Hali hii inatokana na kufiwa na baba yangu mzazi mwaka 2006 na hali ya mama yangu siyo nzuri kutokana na kuumwa na pia hana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato.
“Kutokana na mama yangu kuumwa amekuwa akishindwa kulipa kodi ya nyumba .
“Mimi baada ya kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na kuona hali ya mama ni ngumu nilitafuta wasamaria wema, ikashindikana, nikaenda Serikali ya Mtaa ya Kimara Bucha ambako walinipa barua ya utambulisho ili niende kwa wananchi kuomba msaada.
“Nimetembea sana kwa watu mbalimbali lakini sijapa msaada wowote alisema huku akitokwa machozi.
Yeyote aliyeguswa na habari ya kijana huyu anaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0657864141, yupo Kimara.

No comments:

Post a Comment