Taarifa za kutatanisha
zimeibuka kuhusu afya ya Hosni
Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia
maandamano
ya kutaka mageuzi nchini Misri mwaka jana.
Baadhi ya vyombo vya
habari vimetangaza kuwa uhai wake
unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya
kuhamishwa
kutoka gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini
Cairo.
Mubarak mwenye umri wa
miaka 84 aliugua kiharusi akiwa jela, hali iliosababisha ahamishwe hadi
hospitalini akiwa
mahututi.
Kiongozi huyo aliondolewa
mamlakani mwaka jana kufuatia maandamano ya raia wa nchi hiyo yakupinga utawala
wake.
Mwezi uliopita
alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuamrisha mauaji ya baadhi ya
waandamanaji hao.
Mara kadhaa kumekuwepo na
taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya rais huyo wa zamani lakini kila mara
zimepuuzwa.
Taarifa hizo kuhusu afya
yake zimetokea wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye bustani
ya Tahrir kulaani uamuzi wa baraza la kijeshi wa kujilimbikizia
mamlaka.
Maandamano hayo
yamepangwa na viongozi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood. Mgombea wa kundi hilo
wa kiti cha urais Mohammed Musri anadai kushinda uchaguzi huo uliofanyika
mwishoni mwa wiki.
Lakini pia mpinzani wake
ambaye pia alikuwa waziri mkuu chini ya utawala wa Rais Mubarak, Ahmed Shafiq
naye anadai ushindi.
Matokeo rasmi ya uchaguzi
huo yatatanzagwa alhamisi.
Vuguvugu la Muslim
Brotherhood limeahidi kumfungulia mashtaka mapya Hosni Mubarak punde tu litakapo
pata madaraka na linataka ahukumiwe kifo.
Chanzo - BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment